BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIYM

TAMPRO SACCOS LTD

KWA MIKOPO HALALI, MASHARTI NAFUU!

CHIMBUKO:

Neno TAMPRO ni ufupisho wa maneno “Tanzania Muslim Professionals Association” yakimaanisha Taasisi/Jumuiya ya wanataalama wa kiislam Tanzania iliyosajiliwa mwaka 1997 ikiwa na lengo la kuwaunganisha waislam wote wenye fani au taaluma mbalimbali ili kwa pamoja waweze kutumia taaluma zao kwa maslahi ya Ummah/Jamii hasa ya kiislam.

Katika harakati za kuikomboa jamii ya waislam kiuchumi, TAMPRO ilifanya utafiti wa kina juu ya sababu na athari za hali hii mbaya ya kiuchumi, na kugundua kuwa moja ya mambo yanayoiathiri jamii yetu kiuchumi na kiimani ni suala zima la mfumo wa Fedha unaoendeshwa kwa misingi ya RIBA. Ndipo TAMPRO ikaanzisha TAMPRO SACCOS LTD ikiwa ni Saccos ya kwanza ya kiislam kusajiliwa Tanzania.

Tampro Saccos Ltd ilisajiliwa tarehe 23/04/2010 na kupewa namba ya usajili DSR 1257, na kuzinduliwa rasmi tarehe 09/05/2010. Baadhi ya faida za kuwa mwanachama wa Tampro Saccos Ltd ni pamoja na;

Ø  Kujengewa tabia ya kujiwekea akiba zako mara kwa mara kwa ajili ya maendeleo yako na jamii kwa ujumla.

Ø  Kupata mikopo isiyokuwa na Riba na kwa masharti nafuu.

Ø  Kupata mafunzo ya ujasiriamali, ujasiri binafsi na mfumo wa Fedha wa kiislam.

Ø  Kuunganishwa na benki za kiislam nchini kwa ajili ya huduma mbalimbali za kibenki.

Ø  Kupata nafasi ya kukutana na waislam wengine kutoka sehemu mbalimbali kwa lengo la kufahamiana, kusaidiana pamoja na kunasihiana kuhusu misingi ya uislam.

MASHARTI YA KUWA MWANACHAMA:

Ili uweze kuwa mwanachama unatakiwa kutimiza masharti yafuatayo;

v  Uwe ni muislam unayejitambua kwa kuzingatia na kutekeleza haki na wajibu wako kwa Mwenyezi Mungu.

v  Kulipia malipo yafuatayo;

ü  Kiingilio cha uanachama ambacho kinalipwa mara moja tu ni TZS.20,000/=

ü  Gharama za uendeshaji angalau za miezi 5 ambapo kila mwezi ni TZS.2,000/=

ü  Kununua angalau Hisa 2 ambapo kila hisa ni TZS.5,000/=

ü  Kujiwekea Akiba yako angalau TZS.10,000/=

ü  Gharama ya fomu ya kujiunga TZS.7,000/=

ü  Uwe na picha mbili za paspoti saizi za rangi.

v  Kutafuta wadhamini wawili wenye sifa moja kati ya zifuatazo;

ü  Wanachama wa Tampro au Tampro Saccos.

ü  Maimamu(viongozi wa misikiti) karibu na unapoishi.

ü  Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa unapoishi.

ü  Mwajiri hasa akiwa Muislam

ü  Muislam ambaye unaweza kujiunga nae kwa wakati mmoja.

v  MUHIMU: Kwa muislam mwenye nia ya kujiunga ila ana uwezo mdogo anaweza akaanza kulipia TZS.30,000/= ambayo inajumuisha kiingilio cha uanachama pamoja na Gharama za fomu ya kujiunga. Halafu baadae akawa analipia kidogo kidogo Gharama za uendeshaji, Hisa pamoja na kujiwekea Akiba zake.

MASHARTI NA UTARATIBU WA MIKOPO.

 1. A)

Ili mwanachama aweze kukopeshwa ni lazima atimize masharti yafuatayo;

v  Awe mwanachama  kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu.

v  Awe na akiba zitakazo muwezesha kupata kiasi cha mkopo anachohitaji.

v  Awe anamiliki hisa zisizopungua 24 ambapo kila Hisa ni TZS.5000/=

v  Awe ameshalipia gharama za uendeshaji za mwaka mzima. (TZS.24,000/=)

v  Awe amelipia gharama ya fomu ya mkopo ambayo ni  TZS.5000/=

v  Akiba yake ya mwisho kuiweka iwe imekaa kwenye saccos kwa muda usiopungua mwezi mmoja. (huwezi kuweka akiba leo ukakopa kesho.)

v  Awe amejaza fomu ya maombi ya mkopo kwa ukamilifu.

v  Awe hana mkopo mwingine kwani mkopo juu ya mkopo hairuhusiwi.

 1. B)

Ø  Dhamana ya kwanza kabisa ambayo inazingatiwa na Tampro Saccos ni Imani{TAWHEED} ya mkopaji. Tunaamini kuwa kila mkopaji anafahamu sheria ya uislam kuhusu mikopo na wajibu wake.

Ø  Akiba na hisa zake katika Saccos.

Ø  Mtu binafsi ambaye ni Mwanachama hai wa Tampro au Tampro Saccos asiye na mkopo, Mwajiri wa mkopaji au Muislam yeyote atakaye kubalika na kamati ya mikopo.

Ø  Kwa upande wa wanawake walioolewa, Mume wake ni lazima awe miongoni mwa wadhamini wake.

Ø  Kwa kujiridhisha zaidi kamati ya mikopo inaweza ikahitaji vielelezo vingine kama vile leseni za biashara na/au hati za nyumba au viwanja au vitu vingine vyenye thamani sawa au zaidi ya mkopo unaoombwa.

 1. C) KIASI NA MAREJESHO.
 • Kwa sasa kiasi cha mkopo kinachotolewa kwa wanachama waliotimiza vigezo na masharti ni mara mbili tu ya Akiba ya Mwanachama.
 • Na pia mkopo wa kwanza hauwezi kuzidi TZS.3,000,000/= na ukimaliza kurejesha mkopo wako, baada ya mwezi mmoja unaweza kuomba tena.
 • Mkopo wa juu kabisa wa Fedha Taslimu ni TZS.5,000,000/= ambapo utakopeshwa kiasi hiki baada ya kufanikiwa kukopa si chini ya TZS.3,000,000 na kufanikiwa kuirudisha vizuri.
 • Marejesho ya mkopo yanatakiwa yafanyike kila mwezi kwa muda usiozidi miezi 12(mwaka mmoja) tu. Hivyo utachukua kiasi cha mkopo wako na kugawanya kwa 12 ili kupata kiasi cha chini cha marejesho ya kila mwezi.
 1. D) UTARATIBU WA MIKOPO:

v  Kwa sasa Tampro Saccos inatoa Mikopo (Cheki kwa waombaji waliokubaliwa) mara moja kwa kila mwezi na hasa Jumapili ya kwanza ya kila  mwezi.

v  Wiki ya kwanza ya kila mwezi yaani  tarehe 1 mpaka 7 ni wiki ya kuchukua, kujaza kwa ukamilifu na kurudisha fomu za Mikopo. Baada ya hapo wiki tatu zinazofuata ni kwa ajili ya kuwafuatilia/kuwachunguza waombaji.

MASWALI YANAYOULIZWA MARAKWAMARA KUHUSU SACCOS!

1) SACCOS ni nini?

Saccos ni kifupi  cha  maneno ya kiingereza  Saving &Credit Cooperative Society,  yakimaanisha  chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa.

2) Tampro Saccos  Ltd  ni nini?

Ni  chama cha ushirika cha akiba na mikopo kanachojiendesha kwa kufuata misingi na sheria za dini ya kiislam, kilichoanzishwa na Jumuiya ya Wataalamu wa Kiislam wa Tanzania.

3) Saccos inawezaje kujiendesha bila riba?

Allah  (s.w) alipoharamisha riba, alihalalisha biashara. Hii ina maana kwamba Allah (s.w) anataka watu wajiendeshe au kujiendeleza kupitia biashara (faida) na sio riba.  Kwahiyo  Tampro  Saccos Ltd ina malengo ya kukua na kujiendesha kupitia biashara (miradi) au faida.

Ila katika kipindi hiki cha awali ambapo hakuna miradi, Tampro Saccos Ltd inajiendendesha kupitia michango ya wanachama wake ya kila mwezi (gharama za uendeshaji), viingilio vya wanachama wapya na misaada mbalimbali.

4) Akiba ni nini?

Akiba ni fedha anazoziweka mwanachama kwenye Saccos (angalau tsh.10,000/= kwa mwezi). Lengo kuu la akiba za mwanachama ni kumwezesha kuomba mkopo hapo baadae atakapohitaji.

 1. Hisa ni nini? 

Ni fedha anazoziweka mwanachama kwenye Saccos (angalau Tsh10,000/= kwa mwezi) kwa malengo  makuu mawili:

Kupata umiliki kwa maana ya kuwa na haki na wajibu kama mwana chama halali na hai wa Tampro Saccos Ltd.

Kwa ajili ya uwekezaji kwa maana ya kuanzisha biashara  au miradi mbalimbali itakayo leta faida katika chama ambapo mwisho wa mwaka faida hiyo itagawanywa baina ya Saccos na wanachama wake.

 1. Je mwanachama anaweza kuchukua sehemu ya akiba yake akiwa na dharura?

HAPANA; kama tulivyosema awali kuwa Saccos ni vyama vya kuweka na kukopa, siyo kuweka na kuchukua. Hivyo akiba itatumika kwa ajili ya kukopa tu. Mwanachama anaruhusiwa kukopa ndani ya Akiba yake.

Mwanachama atakayehitaji kuchukua sehemu ya Akiba yake, anatakiwa atoe taarifa ya maandishi kwa muda usiopungua miezi mitatu kabla. Hii ni kwa sababu Akiba za wanachama ndio nguzo kuu ya Saccos yoyote katika kutimiza lengo kuu la kutoa Mikopo kwa wanachama wake.

 1. Je mwanachama anaweza kukopa kutokana na hisa zake?

HAPANA; Mkopo hutokana na akiba ya mwanachama tu. Mwanachama hawezi kukopa wala kuchukua Hisa au hata sehemu ya Hisa zake. Kwani kufanya hivyo ni kujifuta katika chama. Kwahiyo Hisa zitarudishwa pale  mwanachama atakapo hitaji kujifuta/kujiondoa katika chama.

 1. 8. Amana ni nni?

Huu ni mfuko au huduma au fedha anazozihifadhi  mwanachama kwa malengo ya kuzichukua wakati wowote pindi atakapohitaji kutokana na dharura mbalimbali. Maranyingi mfuko huu huwa na Gharama au makato yake yanayojitegemea. Kwa sasa Tampro Saccos Ltd bado haijaanzisha mfuko au huduma hii.

 1. Mwanachama akitaka kujifuta katika chama anafanyaje?

Anaandika barua ya maombi ya kujifuta katika chama  kwa mwenyekiti wa bodi, halafu anasuburi kwa kipindi kisichopungua miezi 3 ili aweze kurudishiwa akiba na Hisa zake.

 1. Kuna  tofauti gani kati ya faida na riba?

Baadhi ya tofauti  kati ya faida na riba kwa mujibu wa sheria za kiislam ni:-

 1. a) Faida inatokana na biashara ambayo inahusisha  bidhaa, Riba hutokana na mkopo au biashara inayohusisha fedha taslimu za sarafu/taifa moja.
 2. b) Faida haiwezi kubadilika kulingana na wakati, Riba inabadilika/ inaongezeka kadri ya muda unavyoongezeka.
 3. c) Uislam unatambua kuwa kuna faida na hasara, lakini Riba haina kinyume chake.(yaani ikipatikana faida utatozwa riba na hasra pia inatozwa riba.)

Kwa maelezo zaidi unaweza kufika katika ofisi yetu iliyopo Magomeni Usalama karibu kabisa na ofisi za manispaa ya Kinondoni. Au piga simu 0787268745, 0715268745 AU 0767268745. Au tumia Email tamprosaccos@gmail.com

TAMPRO SACCOS LTD,

KWA MIKOPO HALALI, MASHARTI NAFUU.

 

KARIBU SANA!